MKUU WA JESHI LA POLISI JENERALI SAIMON SIRRO AMEWATAKA RAIA WAPYA WA BURUNDI KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA UHALIFU
TAREHE 11-12-2017
Mkuu wa jeshi la polisi nchini insipekta jenerali
Saimon Sirro amewataka raia wapya wa Burundi waliokuwa wakiishi katika kambi za
Mishamo na Katumba mkoani Katavi na Ulyankulu mkoani Tabora kujiepusha na vitendo vya uhalifu.
IGP Sirro
ametoa kauli hiyo kufuatia baadhi ya raia hao wapya kujihusisha na vitendo vya
ujambazi wa kutumia silaha, kuingiza silaha kutoka nchini mwao,pamoja na
wahamiaji haramu vitendo ambavyo ni kinyume na sheria za Tanzania.
Sirro amewataka raia hao wapya kuwa wazalendo, raia wema, na washirikiane na watanzania
wenzao kutekeleza shughuli mbalimbali za
maendeleo na yeyote atakayebainika kijihusisha na uhalifu ajue kwamba vyombo
vya ulinzi na usalama vitawafuatilia.
Aidha amewahakikishia wakazi wa mkoa wa Tabora na
nchi nzima kuwa jeshi la polisi limejijenga na liko kamilifu kukabiliana na
uhalifu wa aina mbalimbali hivyo amewataka wananchi kutekeleza kazi zao bila
wasiwasi wowote.
Hata hivyo Sirro yupo mkoani Tabora kukagua kazi
mbalimbali na utendaji kazi wa jeshi la
polisi na kuwahimiza askari wa jeshi hilo kuwatumikia wananchi kwa kuzingatia kanuni,
taratibu na sheriaza nchi.
MKUU WA JESHI LA POLISI JENERALI SAIMON SIRRO AMEWATAKA RAIA WAPYA WA BURUNDI KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA UHALIFU
Reviewed by safina radio
on
December 11, 2017
Rating:

No comments