RAIS WA ZIMBABWE EMMERSON MNANGAGWA ATEUA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI

TAREHE 01-12-2017





Rais mpya wa Zimbabwe Emerson Mnangagwa ameteua baraza jipya la mawaziri linalojumuisha wanachama watiifu kwa chama tawala nchini humo pamoja na maafisa wa jeshi la nchi hiyo ambalo hatua yake ilisaidia kumuondoa madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo Robert Mugabe.

Hata hivyo hakuna mwanasiasa wa upinzani aliyejumuishwa katika baraza hilo jipya ambalo linaonekana kuwa jaribio la kwanza kwa Mnangagwa mshirika wa muda mrefu wa Mugabe, iwapo ataongoza pasipo kivuli cha Mugabe.

Miongoni mwa wanaounda baraza hilo lenye mawaziri 22 lililotangazwa jana jioni kupitia televisheni ya taifa nchini humo ni pamoja na Meja Jenerali Sibusiso Moyo ambaye anakuwa waziri wa mambo ya nje na Chris Mutsvangwa kiongozi wa maveterani wa kivita aliyeteuliwa kuwa waziri wa habari.


Novemba 15 , Moyo alitangaza jeshi kuchukua mamlaka hatua iliyoenda sambamba na Mugabe kuwekwa katika kizuizi cha ndani na baadaye kujiuzulu na kuhitimisha utawala wake uliodumu kwa miaka 37.
RAIS WA ZIMBABWE EMMERSON MNANGAGWA ATEUA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI RAIS   WA  ZIMBABWE EMMERSON MNANGAGWA  ATEUA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI Reviewed by safina radio on December 01, 2017 Rating: 5

No comments