RAIS TRUMP ATANGAZA RASMI KUUTAMBUA JERUSALEM KUWA MJI MKUU WA ISRAEL
TAREHE 07-12-2017
Rais Donald Trump
wa Marekani ametangaza rasmi kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel licha
ya uamuzi huo kupingwa na viongozi kadhaa wa kidunia.
Kufuatia tangazo
hilo la Trump ubalozi wa Marekani sasa utahamishwa kutoka mjini Tel Aviv na
kupelekwa Jerusalem.
Akizungumza katika ikulu ya Marekani White House Trump amesema
ni muda muafaka sasa kuitambua rasmi Jerusalem kama mji mkuu wa Israel na
kuongeza kuwa hatua hiyo ni ishara ya kutambua ukweli uliopo kuhusiana na suala
hilo.
Amesema wakati
alipoingia madarakani aliahidi kuangalia kwa makini changamoto zinazoikabili
dunia na kuwa hauwezi kutafuta suluhisho la matatizo kwa kutumia njia zilezile
zilizoshindwa.
Kufuatia hatua hiyo
katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekosoa hatua hiyo na kusema
hakuna mpango mbadala zaidi ya shirikisho la mataifa mawili,ambapo pia baraza
la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajia kukutana katika kikao cha dharura
ikiwa ni baada ya rais Donald Trump kutangaza uamuzi huo.
RAIS TRUMP ATANGAZA RASMI KUUTAMBUA JERUSALEM KUWA MJI MKUU WA ISRAEL
Reviewed by safina radio
on
December 07, 2017
Rating:

No comments