RAIS TRUMP ATANGAZA MKAKATI WA KITAIFA WA USALAMA.
TAREHE 19-12-2017
Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza mkakati wa kitaifa wa usalama katika utawala wake ambao unaangazia vipaumbele vya kwanza vya Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza mkakati wa kitaifa wa usalama katika utawala wake ambao unaangazia vipaumbele vya kwanza vya Marekani.
Mkakati huo
umesisitiza ukuaji wa kiuchumi na usalama wa taifa hilo kwa kuweka sheria kali
za kulinda mipaka na kuwa na jeshi imara.
Katika hotuba
yake,rais Trump ametaja kuwa China na Urusi ni washindani wanaopinga ushawishi
wa Marekani katika ngazi ya kimataifa.
Licha ya kuwa Marekani
inaongoza kwa kuwa na jeshi lenye nguvu lakini bado wapinzani wake wa kisiasa
na kiuchumi wanahangaika duniani kote ili kuitoa katika mstari huku Marekani
ikiwa inakabiliwa na makundi ya kigaidi,mitandao ya wahalifu na watu wengine
ambao wanachochea vurugu na uovu.
Aidha mkakati huo
unajumuisha ujenzi wa ukuta katika mpaka wa Mexico, kuimarisha sheria za
uhamiaji na kusitisha mpango wa kutoa viza za bahati nasibu.
RAIS TRUMP ATANGAZA MKAKATI WA KITAIFA WA USALAMA.
Reviewed by safina radio
on
December 19, 2017
Rating:
No comments