UJERUMANI YAPUNGUZA UHUSIANO WAKE NA KOREA KASKAZINI.
TAREHE 01-12-2017
Ujerumani
imepunguza uhusiano wake wa kibalozi na Korea Kaskazini baada ya nchi hiyo
kufanya jaribio jingine la kombora la masafa marefu.
Waziri wa mambo ya
nje wa Ujerumani, Sigmar Gabriel amesema akiwa ziarani nchini Marekani kwamba
afisa mmoja wa kibalozi atapunguzwa kutoka kwenye ubalozi wa Ujerumani mjini
Pyongyang.
Waziri Gabriel pia
ameitaka Korea Kaskazini nayo ipunguze idadi ya wawakilishi wake wa kibalozi
waliopo nchini Ujerumani.
Balozi wa Marekani
kwenye Umoja wa Mataifa, Nikki Haley amezitaka nchi zote zivunje uhusiano wao
wa kibalozi na Korea ya Kaskazini.
Pamoja na hayo
Marekani imetishia kuuteketeza utawala wa Kim Jong Un endapo vita vitatokea.
Jumatano iliyopita
Korea Kaskazini ilirusha kombora jipya ambalo linaweza kuifikia nchi yote ya
Marekani.
UJERUMANI YAPUNGUZA UHUSIANO WAKE NA KOREA KASKAZINI.
Reviewed by safina radio
on
December 01, 2017
Rating:

No comments