WABUNGE WA REPUBLICAN NCHINI MAREKANI WAKUMBWA NA KIZINGITI.

20-12-2017
Makamu wa Rais Mike Pence alitangaza matokeo ya kura hizo
Image caption
Wabunge wa Republican nchini Marekani wamekumbwa na kizingiti cha dakika ya mwisho katika juhudi zao za kuidhinisha marekebisho makubwa ya kodi kuwahi kufanywa katika miaka 30, na hivyo wanahitaji kupiga kura tena hii leo,ingawa itachelewesha kile ambacho kingekuwa ni ushindi wa kwanza kabisa bungeni chini ya Rais Donald Trump.

Bunge la Marekani ambalo linadhibitiwa na Warepublican lilipitisha mpango wa kodi jana na kuuwasilisha mswada huo katika baraza la Seneti, ambako afisa mmoja alitoa uamuzi kuwa vipengele vitatu vya mswada huo wa Bunge havikukidhi sheria pana za Seneti.


Kufikia jana jioni, mpango ulikuwa ni Seneti kufuta vipengele hivyo vitatu na kuupigia kura mswada huo,ambapo Ikiwa utaidhinishwa kama inavyotarajiwa, mswada huo  utarejeshwa Bungeni ili kupigiwa tena kura siku ya leo.
WABUNGE WA REPUBLICAN NCHINI MAREKANI WAKUMBWA NA KIZINGITI. WABUNGE WA REPUBLICAN NCHINI MAREKANI WAKUMBWA NA KIZINGITI. Reviewed by safina radio on December 20, 2017 Rating: 5

No comments