MWANASIASA WA CHAMA CHA DEMOCRATS NCHINI MAREKANI APATA USHINDI MKUBWA
TAREHE 13-12-2017
REUTERS

Mwanasiasa
wa chama cha Democrats nchini Marekani Doug (Dag) Jones amepata ushindi mkubwa
leo katika kinyang'anyiro kikali cha kuwania kiti cha Seneti katika jimbo la
Alabama.
Jimbo hilo lilishikiliwa kwa muda mrefu na
chama cha republican na ushindi wa Bw Jones ni pigo kwa rais wa Marekani Donald
Trump .
Roy
Moore wa Republican alishindwa kwa kupata asilimia 48.4 ya kura huku mgombea wa
Demokrat akiibuka na ushindi kwa kupata kura asilimia 49.9.
Jones
mwenye umri wa miaka 63 alikuwa mwendesha mashtaka wa serikali aliyepata
umaarufu baada ya kuwashtaki wanachama wa kundi la imani kali ya kibaguzi Ku
Klux Klan lililoshambulia kanisa moja la watu weusi katika miaka ya 1960 ambapo
wasichana wanne waliuwawa.
MWANASIASA WA CHAMA CHA DEMOCRATS NCHINI MAREKANI APATA USHINDI MKUBWA
Reviewed by safina radio
on
December 13, 2017
Rating:
No comments