WAFUGAJI MJINI SHINYANGA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA UFUGAJI YA MWAKA 2004.

TAREHE 19-12-2017


Wafugaji mjini Shinyanga wametakiwa kuzingatia sheria za ufugaji ya mwaka wa 2004 ambayo inaelekeza kufuga kwa kutumia mazizi vinginevyo watakaokiuka watachukuliwa hatua za kisheria.
`
Kauli hiyo imetolewa na afisa mifugo wa halmashauri ya Manspaa ya Shinyanga Bw Virwan Mwaliko kufuatia mifugo kuzagaa mitaani na kusababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara.

Bw Mwaliko amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya mifugo ya mwaka wa 2004 inasema kuwa mfugaji atakayekiuka sheria hiyo atashtakiwa na adhabu yake ni kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya shilingi elfu 50 au vyote kwa pamoja.


Hata hivyo afisa huyo ameongeza kuwa katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Octoba hadi Disemba mwaka huu jumla ya wafugaji mia moja na tano wamekamatwa na kutozwa faini kwa mujibu wa sheria iliyowekwa.
WAFUGAJI MJINI SHINYANGA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA UFUGAJI YA MWAKA 2004. WAFUGAJI MJINI SHINYANGA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA UFUGAJI YA MWAKA 2004. Reviewed by safina radio on December 19, 2017 Rating: 5

No comments