MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA SAMIA SULUHU HASSAN AHAMIA RASMI MJINI DODOMA.

TAREHE 15-12-2017

Makamu wa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan leo amehamia rasmi mjini Dodoma ikiwa ni mkakati wa serikali ya awamu ya tano ya kuhamishia shughuli zake mkoani humo ambako ndiko makao makuu ya nchi.

Akizungumza mara baada ya kuwasili mkoani humo mjini humo Mh Suluhu amesema kuwa kwa sasa shughuli zote za makamu wa rais muungano na mazingira zitafanyikia mkoani Dodoma  kwa kuwa mawaziri wote wa wizara yake walikuwa ameshatangulia kufika katika makao makuu hayo.

Ameongeza kuwa kwa kuwa ofisi yake inahusika na mambo ya mazingira wameanza kampeni maalumu ya kuufanya mkoa wa Dodoma kuwa wa kijani wa kupanda miti,ambapo kampeni hiyo itazinduliwa Disemba 21 mwaka huu na kuwashirikisha wananchi wote wa mkoa huo.

Kwa upande wake waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kassimu Majaliwa amesema kuwa  serikali inaendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ya mji wa Dodoma ikiwemo barabara na amewataka viongozi pamoja na wananchi kushirikiana serikali katika sekta ya maendeleo ili kuhakikisha manspaa ya  Dodoma inakuwa jiji kubwa hapa nchini.

Hata hivyo mbali na makamu wa rais viongozi wengine ambao wameshahamia mjini Dodoma ni waziri mkuu Mh Majaliwa Kassimu,mawaziri wa wizara zote,makatibu wakuu pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za serikali,ambapo rais Magufuli anatarajiwa kuhamia mjini humo mapema mwakani.


MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA SAMIA SULUHU HASSAN AHAMIA RASMI MJINI DODOMA. MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA SAMIA SULUHU HASSAN  AHAMIA RASMI MJINI DODOMA. Reviewed by safina radio on December 15, 2017 Rating: 5

No comments