WATOTO 4 WAFARIKI KATIKA AJALI NCHINI UFARANSA
TAREHE 15-12-2017

watoto wanne wamefariki dunia huku wengine 20
wakijeruhiwa baada ya basi lao la shule kugongana na treni kusini magharibi mwa
Ufaransa.
Vyombo vya habari
nchini humo vimeripoti kuwa ajali hiyo imetokea kwenye eneo la makutano ya reli
na barabara katika mji ulioko jirani na eneo la mpaka kati ya Ufaransa na
Uhispania.
Watoto hao walio na
umri kati ya miaka 11 na 17 walikuwa wakirejea nyumbani kutoka shule iliyoko
jirani na mji wa Pepinan.
Waziri Mkuu wa Ufaransa, Edward Philipe
amesema uchunguzi kuhusiana na chanzo cha ajali hiyo bado unafanyika.
WATOTO 4 WAFARIKI KATIKA AJALI NCHINI UFARANSA
Reviewed by safina radio
on
December 15, 2017
Rating:
No comments