NIGERIA KUMBADILISHA KAMANDA WA JESHI ANAYEONGOZA VITA DHIDI YA BOKO HARAM
TAREHE 07-12-2017
Serikali ya Nigeria imeamua kumbadilidhsa kamanda wa
jeshi anayeongoza vita dhidi ya kundi la kigaidi la Boko Haram ikiwa imepita
nusu mwaka tu tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo.
Msemaji wa jeshi la Nigeria amethibitisha habari hiyo na
kuongeza kuwa, wimbi la mashambulizi ya magaidi wa Boko Haram limeongezeka sana
hivi sasa, hivyo jeshi limeamua kumbadilisha kamanda aliyekuwa anaogoza vita
dhidi ya genge hilo.
Amesema kuwa Makamanda wa kijeshi huwa wanabadilishwa
mara kwa mara kama njia ya kutoa msukumo mpya katika vita dhidi ya ugaidi
kwenye eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria ambapo uasi wa genge la
wakufurishaji la Boko Haram umeingia katika mwaka wake wa tisa.
Hata hivyo kuzuka wimbi jipya la mashambulizi ya Boko
Haram kunaonesha namna Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria alivyoshindwa
kutekeleza ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi wa rais.
NIGERIA KUMBADILISHA KAMANDA WA JESHI ANAYEONGOZA VITA DHIDI YA BOKO HARAM
Reviewed by safina radio
on
December 07, 2017
Rating:

No comments