JITIHADA YA KUTOA ELIMU ZAIDI YA KUJIKINGA NA MAGONJWA KABLA YA KUUGUA YAHITAJIKA.
TAREHE 19-12-2017.
Katibu mkuu wizara
ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dr Mpoki Wilisibisya
amezitaka taasisi na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayojihusisha na
masuala ya afya kuweka jitihada ya kutoa elimu zaidi ya kujikinga na magonjwa
kabla ya kuugua.
Dr Willsibisya
ameyasema hayo mkoani Geita wakati wa makabidhiano ya vifaa vya watoto njiti
vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 14 iliyotolewa na kampuni ya
Vodacom Foundation hapa nchini katika hospitali ya Chato mkoani Geita.
Amesema kuwa endapo
elimu itatolewa kwa wananchi namna ya kujikinga na magonjwa mbalimbali
itasaidia kuokoa gharama za matibabu pamoja na kuokoa nguvu kazi ya taifa kwa
kuwa mtu akiugua kasi yake ya kufanya kazi inapungua na kinga ni bora kuliko
tiba.
Kwa upande wake
mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dr Ligibati Kausa amesema kuwa,upatikanaji wa
vifaa hivyo utasaidia watoto katika kuwahudumia kiundani zaidi kwa kuwa
watakuwa wamezaliwa kabla ya wakati.
JITIHADA YA KUTOA ELIMU ZAIDI YA KUJIKINGA NA MAGONJWA KABLA YA KUUGUA YAHITAJIKA.
Reviewed by safina radio
on
December 19, 2017
Rating:
No comments