RAIS DONALD TRUMP WA MAREKANI APATA USHINDI MAHAKAMANI.
TAREHE 05-12-2017

Rais
Donald Trump wa Marekani amepata ushindi baada ya majaji wa mahakama ya juu
nchini humo kuamua amri ya marufuku yake ya hivi karibuni dhidi ya wasafiri
kutoka mataifa sita yaliyo na Waislamu wengi kuanza kutekelezwa rasmi.
Mahakama
imebatilisha mapingamizi yaliyokuwa yamewekwa na mahakama za chini ambayo kwa
kiasi fulani yalizuia utekelezaji wa amri hiyo.
Marufuku
hiyo ya muda inayalenga mataifa ya Iran, Libya, Syria, Yemen, Somalia na Chad
huku Korea Kaskazini na baadhi ya maafisa kutoka Venezuela wakiongezwa katika
orodha ya sasa.
Amri
hiyo ya Trump ilikosolewa huku baadhi ya mahakama nchini Marekani zikiamua kuwa
Trump hawezi kuwazuia walio na mahusiano na watu nchini Marekani kutoingia
nchini humo.
RAIS DONALD TRUMP WA MAREKANI APATA USHINDI MAHAKAMANI.
Reviewed by safina radio
on
December 05, 2017
Rating:

No comments