BARAZA LA JUU LA TAIFA NCHINI LIBYA LAPATA MWENYEKITI.
Baraza
la Juu la Taifa la Libya jana lilipiga kura na kumchagua Bw. Khaled al-Meshri kutoka
Chama cha Haki na Ujenzi kuwa mwenyekiti mpya wa Baraza hilo akichukua nafasi
ya Bw. Abdarrahman Swehli.
Duru
za habari zinaeleza kuwa baraza hilo ni chombo cha kutoa ushauri kwa serikali
ya umoja wa kitaifa ya Libya inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa.
Mjumbe
wa Baraza hilo Bw. Musa Faraj amesema kuwa kwa mujibu wa kanuni, mwenyekiti wa
Baraza hilo anachaguliwa kila mwaka.
Hata
hivyo, wajumbe mia moja kumi na tano wa Baraza hilo walipiga kura na Bw. Khaled
al-Meshri alipata kura sitini na nne ambazo ni kura kumi na tisa zaidi kuliko
Bw. Swehli, na wajumbe wengine sita hawakupiga kura.
BARAZA LA JUU LA TAIFA NCHINI LIBYA LAPATA MWENYEKITI.
Reviewed by safina radio
on
April 09, 2018
Rating:
No comments