GUTERRES AMTEUA MEJA JENERALI GEBRE ADHANA WOLDEZGU KUWA KAMANDA UN HUKO ABYEI.
Katibu
mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Antonio Guterres ametangaza kumteua Meja Jenerali
Gebre Adhana Woldezgu kutoka Ethiopia kuwa kamanda mpya wa tume ya Umoja wa
Mataifa huko Abyei, eneo linalogombewa kati ya Sudan na Sudan Kusini.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Antonio Guterres. |
Bw
Guterres amesema Bw Gebre ana uzoefu wa miaka 38 katika jeshi la Ethiopia, na
amewahi kwenda mara kwa mara Sudan, Sudan Kusini, Kenya, Uganda na tume ya
Umoja wa Mataifa nchini Somalia, kwa ajili ya kuimarisha uratibu wa mambo ya
usalama na mipaka wakati akizungumza na wanahabari.
Aidha,
Bw Gebre amechukua nafasi ya Meja Jenerali Tesfay Gidey Hailemichael wa
Ethiopia, ambaye amesifiwa kutoa mchango mkubwa kwa tume hiyo.
Hata
hivyo, amewahi kushiriki kwenye kazi ya upangaji wa operesheni za kulinda amani
za kimataifa na za kikanda.
GUTERRES AMTEUA MEJA JENERALI GEBRE ADHANA WOLDEZGU KUWA KAMANDA UN HUKO ABYEI.
Reviewed by safina radio
on
April 05, 2018
Rating:
No comments