JAMII IMESHAURIWA KUTAMBUA KUWA HOFU NA MASHAKA NI DALILI YA VIFUNGO


Jamii imeshauriwa kutambua kuwa mtu mwenye hofu na mashaka ya kufanya jambo lolote la kimaendeleo katika maisha yake au kutokuwa na kiu ya kusoma na kutafakari neno la Mungu ni mojawapo kati ya dalili za mtu aliyekamatwa na kufungwa vifungo vingi na mwovu shetani.
Image result for HALI YA MASHAKA

Huduma ya redio safina kesho katika ukumbi wa maombi uliopo mbauda jijini Arusha kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa sita mchana imekuandalia maombi maalum ya kuwafungua watu waliofungwa na vifungo mbalimbali ambavyo vimekuwa sababu za wao kutokufikia Baraka walizowekewa na Mungu.


Kwa mujibu wa somo la kesho la kushughulikia vifungo vilivyowafunga watu wasifanikiwe, majira na nyakati za mtu zinaweza kufungwa na shetani ili mtu huyo asiweze kufikia mafanikio yake katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu,afya,kilimo,baishara,ufugaji, pamoja na huduma kwa ujumla.

somo hilo linaeleza kuwa shetani amekuwa akifuwanga watu hasa katika eneo la uchumi,na kuachilia madeni,magonjwa,majeraha ya ndoa, watoto kuacha shule,lakini mtu anapojikita kwenye maombi kwa kutumia neno la Mungu vifungo hivyo hufunguliwa na mtu kuwekwa huru.

Hata hivyo kesho ni siku ya watu kufundishwa jinsi ya kulituma neno la Mungu ili kufungua fungo vyote vinavyowazuia wasiweze kuinuka kiuchumi na kiroho ambapo watu wenye mahitaji mbalimbali wataombewa ili Mungu awaweke huru mbali na vifungo vya shetani.


JAMII IMESHAURIWA KUTAMBUA KUWA HOFU NA MASHAKA NI DALILI YA VIFUNGO JAMII IMESHAURIWA KUTAMBUA KUWA HOFU NA MASHAKA NI DALILI YA VIFUNGO Reviewed by safina radio on April 09, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.