SERIKALI YAANZA KUFUFUA VIWANDA VILIVYOBADILISHWA MATUMIZI.
Serikali kupitia wizara ya viwanda biashara na uwekezaji
imeanza kufufua viwanda vilivyokuwa vimebadilishwa matumizi yake ili kurejesha
shughuli za awali za viwanda hivyo.
STELLA MANYANYA |
Hayo yamesemwa leo bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri
wa viwanda biashara na uwekezaji Mhadisi
Stella Manyanya wakati akijibu swali la mbunge wa Viti maalumu Mariamu Nassoro
Kisangi aliyetaka kujua ni kwa nini baadhi ya viwanda vimebadilishwa matumizi
yake na kuwa maghala ya kuhifadhia vifaa mbali mbali jijini Dar es salaam.
Mhandisi Manyanya amesema kuwa mpango wa serikali ni
kuhamasisha na kuwezesha viwanda visivyofanya kazi viweze kufanya kazi ambapo
uhamasishaji huo wa serikali umewezesha jumla ya viwanda kumi na nane kikiwemo kiwanda cha USI kilichokuwa
kikitengeneza zana za kilimo ambacho kilibadilishwa matumizi na kuwa Tanzania Fillpipe
LTD cha kutengeneza mabomba ya maji.
Aidha, amesema kuwa chini ya kamati maalumu wizara
inaendelea kufuatilia utendaji wa viwanda hivyo vilivyofufuliwa kimoja baada ya
kingine ili viweze kufanya kazi kwa tija.
Hata hivyo, viwanda mia moja hamsini na sita vilibinafsishwa
kwa dhumuni la kutoa ajira, kuzalisha bidhaa zinazokidhi viwango vya kitaifa na
kimataifa na kuongeza mchango wa viwanda katika uchumi wa taifa ikiwa ni
miongoni mwa idadi ya mashirika ya umma mia tatu arobaini na moja yaliyobinafsishwa
na serikali hadi kufikia mwaka 2007.
SERIKALI YAANZA KUFUFUA VIWANDA VILIVYOBADILISHWA MATUMIZI.
Reviewed by safina radio
on
April 09, 2018
Rating:
No comments