asilimia 27 ya vijana wa kike wenye umri kati ya miaka 15-19 hapa nchini wamepata ujauzito.


Naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mh Faustine Ndugulile amesema kuwa asilimia 27 ya vijana wa kike wenye umri kati ya miaka 15-19 hapa nchini wamepata ujauzito.

Image result for picha ya naibu waziri wa afya mh. faustine ndugulile
NAIBU WAZIRI WA AFYA FAUSTINE NDUGULILE
Mh Ndugulile ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu mkoa wa Singida Mh Asha Rose Matende aliyetaka kujua serikali una mpango gani wa kupunguza mimba za utotoni hapa nchini.

Amesema kuwa kutokana na takwimu hizo serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu wameanzisha kampeni maalumu inayomwahamasisha msichana kujitambua inayokwenda kwa jina la “Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima”.

Amefafanua kuwa mbali na kuanzisha kampeni hiyo serikali pia imeanzisha utaratibu wa kutoa elimu kwa mikoa ambayo inaongoza kwa mimba za utotoni ili wananchi wajue madhara yatokanayo na vitendo hivyo ikiwemo vifo vitokanavyo na uzazi pale msichana atakapopata mimba aikiwa na umri mdogo.

Hata hivyo ili kukabiliana na matatizo ya uzazi kwa wanawake katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 serikali imetenga bajeti ya afya ya uzazi kiasi cha shilingi bilioni 18 kutoka shilingi bilioni 5 za awali.



asilimia 27 ya vijana wa kike wenye umri kati ya miaka 15-19 hapa nchini wamepata ujauzito. asilimia 27 ya vijana wa kike wenye umri kati ya miaka 15-19 hapa nchini wamepata ujauzito. Reviewed by safina radio on April 10, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.