VIONGOZI WA VIJIJI WATAKIWA KUANZISHA MADAFTARI YA KUTUNZA KUMBUKUMBU
Jeshi la polisi Mkoani Rukwa limewataka viongozi wa serikali
za vijiji kuanzisha madaftari ya kutunza kumbukumbu ya wakazi wa maeneo yao sanjari
na wageni wanaoingia katika vijji vyao ili kupambana na vitendo vya kihalifu
kwenye maeneo wanayoyaongoza.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA RUKWA GEORGE KIANDO |
Wito huo umetolewa na kamanada wa polisi mkoani
Rukwa Gorge Kiando kufuatia vitendo vya mauaji yaliyokuwa yakiongezeka katika
maeneo yao hususani kwenye wilaya ya Sumbawanga kwenye bonde la ziwa Rukwa.
Aidha wananchi wa maeneo hayo wanawataka baadhi ya viongozi
wa serikali za vijiji wanaokabiliwa na tuhuma hizo kubadili mienendo yao kwa
kuacha tamaa za kutaka kujipatia fedha hizo haraka kwa kuwakumbatia wahalifu.
Mkoa wa Rukwa katika miaka ya hivi karibuni umekuwa
ukiripotiwa vitendo vingi vya mauaji ya vikongwe ambazo zinatokana na tuhuma za
vitendo vya kishirikina sanjari na visa vya wivu wa kimapenzi.
VIONGOZI WA VIJIJI WATAKIWA KUANZISHA MADAFTARI YA KUTUNZA KUMBUKUMBU
Reviewed by safina radio
on
April 10, 2018
Rating:
No comments