KIM JONG UN AZUNGUMZA KATIKA MKUTANO WA CHAMA TAWALA.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amezungumzia hadharani
kwa mara ya kwanza katika mkutano wa chama tawala katika mji mkuu wa nchi hiyo,
Pyongyang.
Rais wa Marekani alikubali mwezi uliopita
kukutana na rais wa Korea Kaskazinii, mkutano ambao utakua wa kwanza katika
historia kati ya rais wa Marekani madarakani na kiongozi wa Korea Kaskazini.
Katika mkutano wa maafisa waandamizi wa chama
cha tawala, Bw Kim walijadili "maendeleo ya sasa kuhusu uhusiano wa Korea
mbili na matarajio ya mazungumzo kati ya Marekani na Korea Kaskazini",
shirika la habari la Korea Kaskazini la KCNA limearifu.
Kim Jong Un alitoa ripoti kuhusu hali inayoendelea
katika rais ya Korea" na hasa mkutano mwingine, uliopangwa kufanyika
mwishoni mwa mwezi huu pamoja na Korea Kusini, kwa mujibu wa shirika la habari
la KCNA.
Trumple alitangaza mwezi uliopita kuwa
alikubali mkutano na rais wa Korea Kaskazini kujadili uwezekano wa kuondoa
silaha za nyuklia katika rasi ya Korea.
KIM JONG UN AZUNGUMZA KATIKA MKUTANO WA CHAMA TAWALA.
Reviewed by safina radio
on
April 10, 2018
Rating:
No comments