MAZUNGUMZO YA AMANI KUHUSU SUDANI KUSINI YANAANZA TENA KATIKA MJI MKUU WA ETHIOPIA ADDIS ABABA
Mazungumzo ya amani nchini Sudan Kusini
yanaanza tena katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Abba.
RIEK MACHAR |
Mazungumzo hayo yanalenga kufikia amani ya
kudumu na makubaliano ya kuachiliwa kwa aliye kuwa makamu wa rais Riek Machar,
ambaye yuko katika kizuizi cha nyumbani nchini Afrika Kusini.
Mazungumzo hayo yanaanza wakati ambapo makundi
mapya ya waasi yanaendelea kuundwa.
Aliyekuwa Mkuu Majeshi nchini humo Paul Malong
ameunda kundi jipya kundi la
waasi,ambapo mkuu huyo alitimuliwa katika wadhifa wake na Rais Salva Kiir mwaka
uliyopita, amechukua hatua hiyo dhidi ya utawala wa Kiir.
Malong ambaye amekuwa akiituhumu serikali kwa
rushwa na makosa yamengine ya ufisadi, amesema kuwa kundi lake litakuwa na
jukumu kubwa la kuiondoa Sudan Kusini kwenye sintofahamu na kuielekeza katika
demokrasia na maendeleo.
Sudan Kusini imeendelea kukumbwa na vita vya
wenyewe kwa wenyewe. Vita hivyo vilianza mwaka mmoja tu baada ya taifa hilo
changa kujipatia uhuru wake.
MAZUNGUMZO YA AMANI KUHUSU SUDANI KUSINI YANAANZA TENA KATIKA MJI MKUU WA ETHIOPIA ADDIS ABABA
Reviewed by safina radio
on
April 10, 2018
Rating:
No comments