BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA KUPIGA KURA LEO.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa huenda likapiga kura
mapema leo kuhusu maazimio kinzani ya Marekani na Urusi ya kuchunguza
mashambulizi ya silaha za sumu nchini Syria, na hivyo kuanzisha mgongano ambao
huenda ukachochea kutumiwa kura za turufu kupinga maazimio hayo yote.
Marekani imewasilisha jana rasimu ya azimio kufuatia madai ya
shambulizi la gesi ya sumu katika mji wa Douma unaodhibitiwa na waasi ambalo
limewaua karibu watu 40 na kumfanya Rais Donald Trump kuashiria kuwa Marekani
huenda ikachukuwa hivi karibuni uamuzi kuhusu hatua ya kijeshi.
Urusi iliwasilisha pendekezo lake mwezi Januari ambalo
limekataliwa na mataifa ya Magharibi yanayosema kuwa linaweza kuipa serikali ya
Syria faida kubwa kuhusiana na uchunguzi unaofanywa ndani ya nchi.
Umoja wa Ulaya na nchi za Magharibi zinautuhumu utawala wa
Rais wa Syria Bashar al-Assad, unaoungwa mkono na Urusi na Iran, kwa kufanya
shambulizi hilo la sumu huku Urusi ikisema hakuna shambulizi lolote la sumu
lililofanywa mwishoni mwa wiki.
BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA KUPIGA KURA LEO.
Reviewed by safina radio
on
April 10, 2018
Rating:
No comments