WANADIPLOMASIA 60 WA MAREKANI WAFUKUZWA NCHINI URUSI


Wanadiplomasia 60 wa Marekani ambao wamefukuzwa kutoka Nchini Urusi baada ya sakata la sumu inayodaiwa kupewa jasusi wa zamani Serguei Skripal na binti yake wameondoka katika ubalozi wa Washington huko Moscow mapema leo.

Image result for PICHA YA BENDERA YA MAREKANI

Mwandishi wa shirika la habari la AFP Alieyeko Moscow ameshuhudia msafara wa mabasi matatu ya ubalozi wa Marekani pamoja na magari mengine yakielekea kwenye uwanja wa kimataifa alfajiri ya leo
Hatua hiyo inakuja baada ya Moscow kuweka tarehe ya Aprili 5 kuwa tarehe ya mwisho kwa wanadiplomasia wa Marekani wawe wameshaondoka nchini humo.
Wiki iliyopita Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov, amesema nchi yake itawafukuza nchini humo wanadiplomasia 60 wa Marekani na kufunga ofisi za ubalozi wake mjini Saint Petersburg kujibu kitendo cha wanadiplomasia wake kufukuzwa na nchi za Magharibi.
Utawala wa Washington wenyewe umesema kuwa kitendo kilichofanywa na Urusi hakina msingi wowote na kwamba Serikali inafikiria hatua nyingine za kuchukua.

WANADIPLOMASIA 60 WA MAREKANI WAFUKUZWA NCHINI URUSI WANADIPLOMASIA 60 WA MAREKANI WAFUKUZWA NCHINI URUSI Reviewed by safina radio on April 05, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.