RAIS WA ZAMANI WA BRAZIL LUIZ INACIO DASILVA AHUKUMIWA MIAKA 12 JELA.
Mahakama Kuu ya Brazil (STF) imemuhukumu rais wa
zamani wa Brazili Luiz Inancio Lula da Silva kifungo cha miaka 12 hukumu
iliyotolewa na majaji 11.
DASILVA |
Mapema siku ya Jumatano Luiz Inacio Lula da
Silva, mwenye umri wa miaka 72, amesema ana matumaini kwamba mahakama ya juu
zaidi nchini humo itakubali hoja ya kutomuweka jela mpaka kukamilika kwa
taratibu zote za kisheria ambapo mahakama ilifutilia mbali ombi hilo kwa kura
sita dhidi ya tano.
Katika uchaguzi wa urais ujao wa mwezi Oktoba,
kiongozi huyo wa mrengo wa kushoto alikuwa anapewa nafasi kubwa ya kushinda.
Maandamano yamefanyika katika miji mbalimbali
ambapo waandamanaji katika mji wa Sao Bernardo wanataka Da silva aachiwe huru.
RAIS WA ZAMANI WA BRAZIL LUIZ INACIO DASILVA AHUKUMIWA MIAKA 12 JELA.
Reviewed by safina radio
on
April 05, 2018
Rating:
No comments