MAADA BIO ATANGAZWA KUWA MSHINDI KATIKA UCHAGUZI WA DURU YA PILI.
Kiongozi wa upinzani nchini Sierra Leone
Julius Maada Bio, ametangazwa na tume huru ya uchaguzi nchini humo kuwa mshindi
wa duru ya pili ya uchaguzi wa rais uliofanyika March 31mwaka huu.
MAADA BIO |
Bw Maada Bio mwanajeshi wa zamani mwenye umri
wa miaka 53 ametangazwa baada ya kushinda nafasi hiyo kwa asilimia 51.81 dhidi
ya mgombea wa chama tawala Samura Kamara aliyepata asilimia 48.19.
Hata hivyo mgombea wa chama tawala Samaura
Kamara amesema atakata rufaa mahakamani kupinga matokeo hayo yaliyotangazwa na
tume huru ya uchaguzi ambayo amesema hayakuzingatia malalamiko yake kuhusu
dosari zilizojitokeza huku akiwatolea wito wafuasi wake kusalia kuwa watulivu
na wenye mshikamano.
Wakati huo huo, Kelele, vifijo na Nderemo
vimesikika jana usiku wakati mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi Nec Mohmaed
Conteh alipotangaza matokeo hayo.
Saa mbili baada ya kutangazwa kwa matokeo
hayo, Julius Maada Bio alikula kiapo pia na kukabidhiwa madaraka kutoka kwa
mtangulizi wake Ernest Bai Koroma ambaye alishinda katika uchaguzi mkuu wa
mwaka 2012.
MAADA BIO ATANGAZWA KUWA MSHINDI KATIKA UCHAGUZI WA DURU YA PILI.
Reviewed by safina radio
on
April 05, 2018
Rating:
No comments