VYANDARUA LAKI MOJA NA ELFU TISINI VYATOLEWA ZANZIBAR.
Waziri wa Afya visiwani Zanzibar Hamad Rashidi
wakati akizindua ugawaji wa vyandarua kwa njia ya kuponi Mjini Unguja amesema
kuwa asilimia sabini ya Wazanzibar ndio wanaotumia vyandarua huku lengo la
Shirika la afya Duniani WHO likiwa ni kufikia asilimia themanini na tano.
Aidha amesema kuwa ugawaji wa vyandarua hivyo vilivyopatikana
umeshaanza kwa walengwa katika vituo vya afya ambapo amewataka wanufaika hao
kuvitumia kwa kufuata maelekezo ya wataalam wa afya.
Hata hivyo, ametahadharisha kwa kusema kuwa serikali
itahakikisha vyandarua hivyo vilivyo gawanywa kwa wananchi haviuzwi bali
vinatolewa bure pamoja na dawa za malaria.
VYANDARUA LAKI MOJA NA ELFU TISINI VYATOLEWA ZANZIBAR.
Reviewed by safina radio
on
April 05, 2018
Rating:
No comments