WAZIRI NCHEMBA AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUWAELIMISHA WAUMINI WAO ILI WAEPUKANE NA UNYANYASAJI.


Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh Mwigulu Nchemba amewaomba viongozi wa dini hapa nchini kuwaelimisha waumini wao ili waweze kuepukana na unyanyasaji wa kijinsia unaofanywa na baadhi ya watu hapa nchini.

Image result for PICHA YA NCHEMBA
WAZIRI NCHEMBA

Mh Nchemba ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu maswali ya wabunge bungeni ambapo amesema kuwa  unyanyasaji wa kijinsia wanaofanyiwa wanawake na watoto unatokana na watu kutokuwa na hofu ya Mungu hivyo endapo viongozi wa dini watatoa elimu hiyo vitendo hivyo vitapungua kwa kiasi kikubwa.

Amesema kuwa ili kukabiliana na hali hiyo serikali imeweka madawati ya kijinsia katika vituo mbalimbali vya polisi hapa nchini hivyo ni vyema watu wanaofanyiwa ukatili huo wakaripoti katika vituo hivyo ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Kwa upande wake naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mh Faustine Ndugulile amesema kuwa ukatili wa kijinsia hufanyika katika ngazi ya familia na kuitaka jamii kutoifumbia macho vitendo hivyo kwani serikali inaendelea kuwachukulia hatua watu kama hao.

Hata hivyo bunge la 11 mkutano wa 11 na kikao cha tatu linaendelea mjini Dodoma ambapo wabunge wanaendelea kujadili bajeti ya waziri mkuu ya mwaka wa 2018/2019 aliyoiwasilisha siku ya jana.

WAZIRI NCHEMBA AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUWAELIMISHA WAUMINI WAO ILI WAEPUKANE NA UNYANYASAJI. WAZIRI NCHEMBA AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUWAELIMISHA WAUMINI WAO  ILI WAEPUKANE NA UNYANYASAJI. Reviewed by safina radio on April 05, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.