RAIS MAGUFULI KUWA MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI WA NYUMBA ZA POLISI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa nyumba za polisi
utakaofanyika tarehe 7 mwezi huu katika uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid
Mkoani Arusha.
RAIS MAGUFULI |
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari Kamanda
wa polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna wa polisi DCP Charles Mkumbo amesema
kuwa uzinduzi huo utaenda sambamba na maonesho mbalimbali ya jinsi jeshi la
polisi linavyofanya kazi za kuhudumia wananchi.
Vilevile Kamanda Mkumbo amesema kuwa sambamba na
uzinduzi huo pia Mh.Rais ataongoza zoezi la ufunguzi wa vituo viwili vya polisi
kikiwemo kituo cha utalii na diplomasia ambacho ni cha kwanza kujengwa nchini
pamoja na kituo cha kisasa cha daraja la kati ambacho kitatoa huduma katika Kata
ya Muriet Mkoani hapa.
Kamanda Mkumbo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza
kwa wingi katika kushuhudia maonesho hayo ambapo amesema tukio hilo
halitoathiri kufanyika kwa shughuli nyingine za kijamii hususan huduma za
barabarani.
Hata hivyo uzinduzi wa nyumba hizo unafanyika
kutokana na kujengwa kwa nyumba mpya za jeshi la polisi baada ya
kuungua kwa nyumba za awali za askari polisi mnamo tarehe 27 mwezi wa 9
mwaka jana,janga ambalo lilisababisha kuteketea kwa mali zote za askari hao.
RAIS MAGUFULI KUWA MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI WA NYUMBA ZA POLISI.
Reviewed by safina radio
on
April 05, 2018
Rating:
No comments