ZAIDI YA WAKAZI 2000 WATAFAIDIKA NA HUDUMA ZA TANESCO BAADA YA KUFUNGULIWA KWA OFISI ZAKE.


Zaidi ya wakazi elfu mbili wa kata ya Madibira Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya wataondokana na adha ya kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilometa themanini kutafuta huduma za TANESCO kutokana na Shirika hilo kufungua ofisi sehemu ya karibu inayowawezesha wananchi wote kupatiwa huduma kwa ukaribu.


Image result for TANESCOAkizungumza baada ya kufunguliwa kwa ofisi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mbarari Rubene Mfune amewaonya wananchi wa wilaya hiyo kuacha mara moja kulalamika kwani serikali inajua matatizo yao.

Naye, Meneja wa TANESCO mkoa wa Mbeya Mhandisi Benedikti Bahati amesema kuwa shirika hilo litaendelea kusogeza huduma kwa wananchi hasa maeneo ya vijijini.

Kwa upande wa baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa baada ya kufunguliwa ofisi hizo za TANESCO katika eneo hilo kunaleta matumaini mapya ya kuwa na uhakika wa huduma tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Hata hivyo, wananchi hao wamesema kuwa awali walikuwa wakifuata huduma za TANESCO mjini Lujewa jambo lililokuwa linasababisha maendeleo yao kurudi nyuma.

ZAIDI YA WAKAZI 2000 WATAFAIDIKA NA HUDUMA ZA TANESCO BAADA YA KUFUNGULIWA KWA OFISI ZAKE. ZAIDI YA WAKAZI 2000 WATAFAIDIKA NA HUDUMA ZA TANESCO BAADA YA KUFUNGULIWA KWA OFISI ZAKE. Reviewed by safina radio on April 04, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.