SHINYANGA NA TABORA ZALENGA KUNUSURU MIKOA HIYO KUGEUKA KUWA JANGWA KWA UPANDAJI MITI.


Mikoa ya Shinyanga na Tabora imetangaza kuanza mpango maalumu wa kugawa miche ya miti kila kaya iliyokabiliana na ukame katika mikoa hiyo.

Image result for miche ya miti
Miche ya Miti.
Wakizungumza mara baada ya zoezi la upandaji miti Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Wakuu wa Mikoa hiyo Zainabu Telack wa Shinyanga na Agrey Mwanri wa Tabora wamesema kuwa hatua hiyo inalenga kunusuru mikoa hiyo kugeuka kuwa jangwa.

Aidha, Wakuu hao wamekutana katika kijiji cha Mwatuju ikiwa ni hatua ya kunusuru ukame katika mikoa hiyo wakati wa kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya upandaji miti kitaifa yanayotarajiwa kufanyika tarehe tano mwezi huu Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Hata hivyo Kauli mbiu ya maadhimisho ya upandaji miti kitaifa ni Tanzania ya viwanda inawezekana, panda miti kwa maendeleo ya viwanda.

SHINYANGA NA TABORA ZALENGA KUNUSURU MIKOA HIYO KUGEUKA KUWA JANGWA KWA UPANDAJI MITI. SHINYANGA NA TABORA ZALENGA KUNUSURU MIKOA HIYO KUGEUKA KUWA JANGWA KWA UPANDAJI MITI. Reviewed by safina radio on April 04, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.