MUHAGAMA AWATAKA VIJANA KUJIUNGA KATIKA VIKUNDI ILI KUFAIDI ASILIMIA TANO YA FEDHA ZA SERIKALI.
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera bunge ajira
vijana na watu wenye ulemavu Mh Jeenister Mhagama amewataka vijana hapa nchni
kujiunga kwenye vikundi mbalimbali vya SACCOS katika maeneo yao ili waweze
kufaidika na fedha za asilimia tano zinatolewa na serikali katika kila
halmashauri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Ajira Vijana na Watu Wenye Ulemavu Mh Jeenister Mhagama |
Mh Mhagama ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma
wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalumu kutoka mkoa wa
kigoma Mh Josephine Gezebuke aliyetaka kujua vijana wanapataje asilimia tano za
fedha zinazotengwa na halmashauri zao kama ilivyoagizwa na serikali .
Amesema kuwa njia rahisi ya vijana kukopeshwa fedha
hizo ni kujiunga na SACCOS zilizoanzishwa katika halmashauri zao na hiyo
itasaidia vijana kuanzisha shughuli mbalimbali za ujasiriamali kwa ushirikiano
kuliko kumkopesha kijana mmoja mmoja.
Ameongeza kuwa fedha ambazo ni asilimia tano kwa
vijana na asilimia tano kwa wanawake hutengwa na halmashauri kwa ajili ya
kusaidia makundi hayo kujikwamua na umaskini.
Hata hivyo mkutano wa 11 bunge la 11 linaendelea
mjini Dodoma likiwa ni maalumu kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti katika
mwaka wa fedha wa 2018/2019.
MUHAGAMA AWATAKA VIJANA KUJIUNGA KATIKA VIKUNDI ILI KUFAIDI ASILIMIA TANO YA FEDHA ZA SERIKALI.
Reviewed by safina radio
on
April 04, 2018
Rating:
No comments