SERIKALI YA CONGO YASEMA MONUSCO INAPASWA KUONDOKA NCHINI HUMO IFIKAPO 2020.
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
inataka kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Kongo, MONUSCO
kuondoka nchini humo ifikapo mwaka 2020.
Jeshi la Umoja wa Mataifa la Kuleta Amani-MONUSCO nchini DRC. |
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kongo, Leonard She
Okitundu amesema hayo baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wiki
iliyopita kupiga kura ya kuongeza mamlaka ya kikosi hicho kwa mwaka mmoja
zaidi.
She Okitundu amewaambia waandishi habari mjini
Kinshasa kuwa wamelijulisha baraza hilo kwamba mamlaka ya sasa ndiyo ya mwisho,
kabla ya kikosi hicho hakijaondoka Kongo baada ya kuwepo nchini humo kwa miaka
20.
Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu kuongezeka kwa
mzozo wa kibinaadamu nchini Kongo, huku kiasi ya Wakongo milioni 13.1 wakiwa
wanahitaji msaada.
Hata hivyo Waziri huyo amethibitisha kuwa Kongo
haitohudhuria mkutano wa wafadhili ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa na Umoja wa
Ulaya ambao umepangwa kufanyika Geneva Aprili 13.
SERIKALI YA CONGO YASEMA MONUSCO INAPASWA KUONDOKA NCHINI HUMO IFIKAPO 2020.
Reviewed by safina radio
on
April 04, 2018
Rating:
No comments