SAAD GADAFFI AFUTIWA MASHITAKA.


Mahakama ya Tripoli imefuta kesi ya mauaji iliyokua ikimkabili Saadi Gaddafi, mtoto wa tatu wa aliyekua rais wa Libya, Muammar Gaddafi.
Saadi Gaddafi amefutiwa mashtaka yote dhidi yake katika kesi ya mwanamichezo Bachir al-Rayani ambaye alifariki dunia mnamo mwaka 2006 baada ya kupigwa kichwani.
Image result for PICHA YA SAADI GADDAFI
SAAD GADAFFI.
Bachir Rayani alifariki dunia baada ya malumbano katika nyumba inayomilikiwa na Saadi Gaddafi.
Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, mahakama imerejelea hukumu za maafisa wa zamani wa Libya baada ya kuhamishwa kutoka gereza la al-Hadaba kwenda sehemu iliyo chini ya usimamizi wa Wizara ya Sheria.
Kwa mujibu wa waangalizi kadhaa, uamuzi huu unaonekana kuwa ni utabiri wa kukabiliana na kesi nyingine za wakuu wa serikali ya zamani ya Libya, ambao wamekuwa wakisubiri haki kwa miaka kadhaa.
Hata hivyo Familia ya Bachir al-Rayani, imepinga uamuzi huo na kuelezea masikitiko yake kwa maelezo kuwa wana  ushahidi wa Saadi Gaddafi kuhusika katika kifo hicho.

SAAD GADAFFI AFUTIWA MASHITAKA. SAAD GADAFFI AFUTIWA MASHITAKA. Reviewed by safina radio on April 04, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.