RAIS WA UTURUKI KUKUTANA NA RAIS WA URUSI NA IRAN.


Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anatazamia kuwapokea leo Jumatano marais wenzake washirika wawili muhimu wa Syria kutoka Irani, Hassan Rohani, na Urusi, Vladimir Putin,.
Image result for picha ya rais recep tayyip wa uturuki
ERDOGAN RAIS WA UTURUKI.
Taarifa zinaeleza kuwa Viongozi hao watajadili mustakabali wa Syria iliyoharibiwa na vita kwa muda wa miaka saba.
Viongozi hao watatu ni washirika muhimu wa rais wa Syria Bashar Al Assad ambapo  Mkutano huo ni uendelezaji wa mchakato wa Astana, ambao haujumuishi Washington na unakinzana na mazungumzo ya Umoja wa Mataifa.
Mchakato huu, uliozinduliwa na nchi hizi tatu mnamo mwezi Januari 2017, ulipelekea kufikiwa makubaliano kuhusu kutengwa kwa maeneo manne yanayokabiliwa na vita  nchini Syria.
 Hata hivyo suala la kutafuta suluhu ya mgogoro wa Syria, ambapo upinzani wa Syria umeendelea kugawanyika na kuwa dhaifu, limeendelea kuzua tofauti ya maslahi kati ya Moscow, Ankara na Tehran.

RAIS WA UTURUKI KUKUTANA NA RAIS WA URUSI NA IRAN. RAIS WA UTURUKI KUKUTANA NA RAIS WA URUSI NA IRAN. Reviewed by safina radio on April 04, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.