WHITE HOUSE YASEMA JESHI LAKE HAINA MUDA RASMI WA KUONDOKA SYRIA.
Ikulu
ya Marekani White House imesema kuwa hakuna muda rasmi uliopangwa kwa vikosi
vya nchi hiyo kuondoka nchini Syria, ingawa rais wa Marekani ameonyesha nia ya
kuondoa haraka jeshi la nchi hiyo nchini Syria.
Ikulu ya White House. |
Msemaji
wa ikulu ya Marekani Sarah Sanders amesema, rais Donald Trump wa nchi hiyo
anaangalia uwezekano wa kushinda vita hiyo kihalisi, na sio kuweka idadi kubwa
ya askari nchini Syria.
Wakati
huohuo, wizara ya ulinzi ya Marekani na wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo
zimeeleza wasiwasi wao kuwa juhudi za muda mrefu zinahitajika ili kulishinda
kikamilifu kundi la wapiganaji la IS.
Hata
hivyo, mpaka sasa, jumla ya askari 2,000 wa Marekani wako nchini Syria.
WHITE HOUSE YASEMA JESHI LAKE HAINA MUDA RASMI WA KUONDOKA SYRIA.
Reviewed by safina radio
on
April 05, 2018
Rating:
No comments