ZAIDI YA EKARI MILIONI MOJA ZA MITI HUVUNWA KILA MWAKA NCHI NA KULETA HOFU YA KUTOKEA KWA JNGWA.


Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamis Kigwangala ameagiza Wakala wa Misitu Nchini TFS kuandaa tathmini ya uvunaji wa miti itakayoonyesha kiwango cha misitu inayofaa kuvunwa ili kupunguza kasi ya uvunaji wa misitu isiyokuwa na manufaa.

Image result for Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamis Kigwangala.
Dk. Kigwangala ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya upandaji miti kitaifa yaliyofanyika wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga ambapo amesema kuwa zaidi ya ekari milioni moja huvunwa kila mwaka hali inayotishia Taifa kugeuka kuwa jangwa endapo uvunaji huo hautadhibitiwa.

Image result for MISITU
Uvunaji misitu.
Image result for MISITU
Ukataji miti.
Waziri Kigwangala ameungana na wakuu wa Mikoa ya Shinyanga na Tabora katika maadhimisho hayo kwa kupanda miti katika eneo la Hospitali ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.

Aidha, kauli mbiu ya maadhimisho hayo ya siku ya upandaji miti kitaifa mwaka huu yaliyofanyika mkoani humo ni Tanzania ya viwanda inawezekana, panda miti kwa maendeleo ya viwanda.

ZAIDI YA EKARI MILIONI MOJA ZA MITI HUVUNWA KILA MWAKA NCHI NA KULETA HOFU YA KUTOKEA KWA JNGWA. ZAIDI YA EKARI MILIONI MOJA ZA MITI HUVUNWA KILA MWAKA NCHI NA KULETA HOFU YA KUTOKEA KWA JNGWA. Reviewed by safina radio on April 05, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.