WAZIRI NDALICHAKO AIONYA TAMONGSCO KUTOAJIRI WALIMU KUTOKA NJE YA NCHI WASIO NA SIFA.


Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako amewaonya wamiliki wa shule binafsi nchni ambao wamekuwa wakiwaajiri walimu kutoka nje ya nchi wasiokuwa na vibali vya kuishi nchini kufuata sheria za nchi.

Image result for Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako.
Waziri Ndalichako ameyasema hayo Mjini Dodoma wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Wamiliki na Mameneja wa Shule za Msingi na Sekondari binafsi TAMONGSCO.

Aidha, Prof. Ndalichako ameongeza kuwa miongoni mwa walimu hao wanaoajiriwa kutoka nje ya nchi wamebainika kukosa sifa za wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi hapa nchini.

Pia  Mkutano huo uliowakutanisha Wamiliki hao wa Shule Binafsi za Msingi na Sekondari unajadili namna ya kuongeza kiwango cha ufaulu katika shule hizo.

Kwa upande wa baadhi ya wamiliki hao wameiomba serikali kuwapunguzia kodi ili nao waweze kushusha ada kwa wazazi wanaowasomesha watoto wao katika taasisi binafsi za elimu.

WAZIRI NDALICHAKO AIONYA TAMONGSCO KUTOAJIRI WALIMU KUTOKA NJE YA NCHI WASIO NA SIFA. WAZIRI NDALICHAKO AIONYA TAMONGSCO KUTOAJIRI WALIMU KUTOKA NJE YA NCHI WASIO NA SIFA. Reviewed by safina radio on April 05, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.