MAGUFULI AZINDUA UKUTA ULIOJENGWA NA JKT KATIKA MACHIMBO YA MERERANI MANYARA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John
Magufuli amezindua ujenzi wa ukuta unaozunguka maeneo ya machimbo ya madini ya
TANZANITE eneo la Mererani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Dk. Magufuli amelipongeza jeshi la kujenga taifa JKT
kwa kazi nzuri ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo huku akiwahidi kuwaajiri
katika nyanja mbali mbali za sekta ya ulinzi kutokana na kazi waliyoifanya.
Kwa upande wake, Waziri wa Madini Mh. Anjela Kairuki
amesema kuwa kwa sasa Wizara madini imeanza kuandaa Kanuni na Taratibu za eneo
hilo la Machimbo ya Madini ya TANZANITE Mererani Control Area, pamoja na
taratibu nyinginezo ikiwemo vitambulisho vya wafanyakazi na uthaminishaji wa
madini hayo.
Naye Waziri wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa Dk. Hussein Mwinyi amesema Jeshi hilo liko tayari kutekeleza maagizo
yoyote ya serikali na utekelezaji wa miradi ya kitaifa kwa maendeleo ya nchi.
Hata hivyo lengo la ujenzi wa mradi wa ukuta huo wa
Mererani katika machimbo ya TANZANITE ni
kudhibiti upotevu wa mapato ya ndani ya nchi.
MAGUFULI AZINDUA UKUTA ULIOJENGWA NA JKT KATIKA MACHIMBO YA MERERANI MANYARA.
Reviewed by safina radio
on
April 06, 2018
Rating:
No comments