URUSI NA SIRYA ZASHTUMIWA NA MAREKANI KUKIUKA MKATABA WA KUSITISHA MAPIGANO MASHARIKI MWA GHOUTA.
WASHINGTON.
Marekani imeishtumu Urusi na serikali ya Syria kwa kukiuka
mkataba wa kusitisha mapigano Mashariki mwa Ghouta, licha ya kupitishwa kwa
azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
![]() |
Ikulu ya Marekani White House. |
Marekani inasema mapigano yanayoendelea kushuhudiwa katika ngome
hiyo ya upinzani, ni ishara tosha kuwa azimio hilo lililopitishwa Jumamosi
iliyopita,halijaheshimiwa.
Katika mkataba ilikubaliwa kuwa, vita vingesitishwa kwa muda wa
siku 30 katika ngome hiyo ya upinzani ili kuruhusu misaada ya kibinadamu
kuwafikia waathiriwa wa vita vinavyoendelea.
Urusi ambayo inasaidia Syria, imeamua kuwa usitishwaji wa
mapigano utadumu kati ya saa tatu asubuhi hadi saa nane mchana, ili kuwaruhusu
raia wa kawaida kuondoka katika ngome hiyo ya upinzani.
Kauli hiyo ya Marekani imekuja wakati huu wakati mashirika ya
kutetea haki za binadamu yakisema kuwa raia wa kawaida wapatao mia sita
waliuawa mwezi Februari katika ngome ya upinzani ya Ghouta.
URUSI NA SIRYA ZASHTUMIWA NA MAREKANI KUKIUKA MKATABA WA KUSITISHA MAPIGANO MASHARIKI MWA GHOUTA.
Reviewed by safina radio
on
March 01, 2018
Rating:

No comments