WANAJESHI WANNE WA KULINDA AMANI WA UMOJA WA MATAIFA WAUAWA NA WENGINE WANNE KUJERUHIWA VIBAYA, MALI.
BAMAKO.
Wanajeshi wanne wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa
wameuawa na wengine wanne kujeruhiwa vibaya katika mlipuko wa mgodi katikati
mwa nchi ya Mali.
![]() |
WANAJESHI WA UN WAFA KWA MLIPUKO MALI. |
Vyanzo vya kiusalama vimesema mlipuko huo ulitokea majira ya
alasiri wakati gari lililokuwa limewabeba askari zaidi ya kumi wa umoja wa
mataifa lilipokanyaga kitu kinachosadikiwa kuwa kilipuzi kati ya maeneo ya Boni
na Douentza katika kanda ya Mopti, katikati mwa nchi hiyo.
Afisa wa jeshi la serikali ya Mali ameviambia vyombo vya habari
kwamba janga hilo jipya limefanya idadi ya askari wa kikosi hicho cha kulinda
amani ambao wamepoteza maisha nchini Mali tangu mwanzo wa mwaka huu kufikia
nane.
Umoja wa mataifa umesema wanajeshi wake wamekuwa wakikabiliwa na
hali ngumu ya kudhibiti mashambulizi ya aina hiyo, kwa kuwa hadi sasa imekuwa
kama kitendawili kumtambua adui anayetekeleza aina hiyo ya mashambulizi kwa
kutumia vilipuzi.
WANAJESHI WANNE WA KULINDA AMANI WA UMOJA WA MATAIFA WAUAWA NA WENGINE WANNE KUJERUHIWA VIBAYA, MALI.
Reviewed by safina radio
on
March 01, 2018
Rating:

No comments