NGWIRA ASEMA SERIKALI INAZINGATIA MAHITAJI YA MAKUNDI MAALUMU.
ARUSHA.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi Anna Ngwira amesema
kuwa serikali ya awamu ya tano kupitia wizara ya Afya inazingatia mahitaji ya
makundi maalum wakiwemo wazee na watoto hivyo ameziagiza halmashauri zote
nchini kuangalia uwezekano wa kuwapatia wabibi wote Bima ya Afya.
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi Anna Ngwira. |
Ameyasema hayo leo wakati akifunga Kongamano la
Kitaifa la Bibi Tanzania lililofanyika Mkoani hapa ambapo Bi.Ngrwira amesema
kuwa utoaji wa bima hizo utakuwa ni
mchango muhimu wa serikali kwa kazi wanayoifanya akina bibi hao katika malezi ya
kuwalea wajukuu ambao wameachiwa kuwalea kutokana na wazazi wao kufariki kwa
sababu mbalimbali.
Amesema kuwa kutokana na kutokuwepo kwa malipo ya
uzeeni kwa wazee hao amezitaka Halmashauri husika kuwapa kipaumbele wabibi wanaolea watoto hao katika mgao wa
fedha kupitia miradi ya vijana na
wanawake itokanayo na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya kila Halmashauri kama
sheria inavyoelekeza.
Aidha amelitaka Shirika la MWEDO pamoja na wadau
wote waandaaji wa kongamano hilo kufuatilia na kuhakikisha huduma hizo zinatolewa
kwa akina mama na kwa wabibi sambamba na kufuatilia kila Halmashauri ambazo
wanatoka wabibi hao ili kuwawezesha kuhudhuria makongamano kama hayo.
Awali akisoma risala kwa niaba ya wabibi waliohudhuria
katika kongamano hilo Bibi Edisi Tarimo amesema kuwa wabibi ni nguzo ya Taifa
la Tanzania hivyo wanahitaji malipo ya uzeeni kwa wazee wote,njia za usaidizi
kwa ajili ya mikopo binafsi ya kibiashara, kuwalinda dhidi ya ukatili na
unyanyasaji na ubaguzi.
NGWIRA ASEMA SERIKALI INAZINGATIA MAHITAJI YA MAKUNDI MAALUMU.
Reviewed by safina radio
on
March 01, 2018
Rating:

No comments