WAASI 5 WA BOKO HARAM WAUAWA NCHINI NIGERIA
Jeshi
la Nigeria limesema limewaua waasi watano wa kundi la Boko Haram katika jimbo
la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria, na kuwaokoa mateka mia moja arobaini
na tisa (149).
Msemaji
wa jeshi la Nigeria Bw. Nwachukwu amesema kuwa jeshi la Nigeria lilifanya operesheni ya
kuwaondoa waasi waliosalia wa kundi la Boko Haram karibu na ngome yake kuu ya
zamani iliyoko kwenye msitu wa Sambisa.
Aidha,
Bw. Nwachukwu amesema kuwa katika operesheni hiyo wamewaua waasi watano na wengine watano wamekamatwa na mateka mia
moja arobaini na tisa (149) wameokolewa.
Hata
hivyo, msemaji huyo ameongeza kuwa kati ya mateka hao 149 kuna wanawake 54 na
watoto 95, ambao hivi sasa wamepelekwa katika kituo cha afya kwa ajili ya
matibabu.
WAASI 5 WA BOKO HARAM WAUAWA NCHINI NIGERIA
Reviewed by safina radio
on
April 09, 2018
Rating:
No comments